Thursday, November 22, 2012

HII NDO CCM " KIKWETE ALONGA NA WANANCHI

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Mkutano Mkuu wa chama kinachotawala nchini Tanzania CCM unamalizika leo huko Dodoma, ambapo miongoni mwa mambo yaliyojitokeza katika siku ya mwisho hii leo ni suala la amani na katiba mpya hususan visiwani Zanzibar

Akizungumza kwenye mkutano huo Mmwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete amesema serikali yake haitakuwa tayari kuona amani inavurugwa.
Kikwete amesema kumekuwa na tabia ya watu kuwalazimisha wenzao kutoa aina ya maoni kwenye tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya na kusema kuwa wale wote wanaofanya hivyo watashughulikiwa vilivyo.
Tamko la rais huyo wa Tanzania limejitokeza kufuatia mada iliyowasilishwa na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais serikali ya zanzibar Mohamed Aboud juu ya hali ya usalama visiwani humo.
Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein  
Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein
Baadhi ya wajumbe na viongozi waandamizi kutoka zanzibar wamesema baada ya Rais wa visiwa hivyo Dr Ali Mohamed Shein kukabidhiwa wadhifa wa umakamu mwenyekiti suala la kitisho dhidi ya serikali ya umoja wa kitaifa litashughulikiwa vilivyo.
Imekuwa ikielezwa kuwa Dr Shein alikuwa kafungwa mikono kwa kutokuwa na kofia ya umakamu, na hivyo kushindwa kusimamia kwa yale anayoyaamini juu ya serikali ya umoja visiwani humo.
Mjumbe wa halmashauri kuu kutoka zanzibar Khadija Hassan Aboud amesema kuwa watatumia vikao vyao wakiwa na hamasa ya uongozi mpya wa ccm visiwani humo kuwashughulikia wale watakaobanika kuchangia hali tete.
Uchaguzi wa Mwenyekiti
Baadaye hii leo unafanyika uchaguzi wa mwenyekiti, pamoja na makamu wawili, halikadhalika kutangazwa kwa matokeo ya nafasi 20 za wajumbe wa nec.Hata hivyo tayari matokeo hayo yamejulika ijapo si rasmi.
Kwa upande wa bara, miongoni mwa wale wanaosemeknana kushinda ni pamoja na Stephen Wasira aliongoza akifuatiwa na Januari Makamba, huku Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akiponea chupuchupu kwa kushika nafasi ya tisa.
Waziri wa Nje Bernard Membe alishindwa kuwemo kwenye kundi la tano bora kwa kukamata nafasi ya sita. Kwa upande wa zanzibar miongoni mwa waliyoshinda ni pamoja na Mohamed Seif Khatib. Kati ya viti hivyo 20 ni wanawake watatu tu waliyoshinda.Hata hivyo matokeo rasmi yatatangazwa baadaye.

No comments:

Post a Comment